Wednesday, June 15, 2011

LEO ni siku ya kupatwa kwa MWEZI

kwa wale waliozaliwa mbele baada ya mwaka 2000,leo ni siku watakayoandika historia mpya katika maisha yao,kupatwa kwa mwezi "moja kwa mojamoja-total lunal eclipse" kati ya matukio ya kushangaza na adimu litatukia usiku wa leo! Mwezi utaenda kati ya jua na dunia kwa takribani dakika 120!kwa kawaida tukio hili huchukua takribani dakika ishirini
 dunia itashuhudia tena kupatwa kwa mwezi kwa moja kwa moja yaani "total lunal eclipse" desemba mwaka huu

nchi mpya hujengwa kwa mawazo mapya!

Takwimu zinatuonyesha kuwa waletao mabadiliko katika jamii ni wale tu wanaochagua kuamka na kuifanyia kazi ndoto nzuri ya mafanikio waliyotoka kuiota!kuota na kutofanyia kazi ulichokiota ni sawa na kuendelea kulala tu!mabadiliko huletwa na vitendo,maneno ni mwanzo tu wa kukufanya utambue jukumu halisi lililo mbele yako,walisema watu wa zamani kuwa "kuchagua kutokuchagua ni sawa na kutokuchagua kabisa" tunatambua nguvu iliyoko kwenye mawazo yetu,kwanini basi tusiyaruhusu yajidhihirishe kwa vitendo?tukichagua kulalamika tutaendelea kuletewa sababu zitakazotufanya tuendelee kulalamika siku zote!wakati umefika basi tuweke kituo kikubwa kuashiria mwisho wa huu "ukichaa unaojirudia" tuanzishe mwanzo mpya na tujenge nchi yetu kwa umoja!mabadiliko ya kweli siku zote huletwa na mapinduzi ya umoja wa kweli usio na kificho,woga,wala kulegalega!
katika ukurasa huu basi,tutapata nafasi  ya kushirikian kupeana habari kwa uwazi wa hali isiyo ya kawaida,usiobagua ila unaozingatia UKWELI TU!
karibuni "and lets make MTANZANIA MWENZANGU Tanzanias most read blogg!