Wednesday, June 15, 2011

nchi mpya hujengwa kwa mawazo mapya!

Takwimu zinatuonyesha kuwa waletao mabadiliko katika jamii ni wale tu wanaochagua kuamka na kuifanyia kazi ndoto nzuri ya mafanikio waliyotoka kuiota!kuota na kutofanyia kazi ulichokiota ni sawa na kuendelea kulala tu!mabadiliko huletwa na vitendo,maneno ni mwanzo tu wa kukufanya utambue jukumu halisi lililo mbele yako,walisema watu wa zamani kuwa "kuchagua kutokuchagua ni sawa na kutokuchagua kabisa" tunatambua nguvu iliyoko kwenye mawazo yetu,kwanini basi tusiyaruhusu yajidhihirishe kwa vitendo?tukichagua kulalamika tutaendelea kuletewa sababu zitakazotufanya tuendelee kulalamika siku zote!wakati umefika basi tuweke kituo kikubwa kuashiria mwisho wa huu "ukichaa unaojirudia" tuanzishe mwanzo mpya na tujenge nchi yetu kwa umoja!mabadiliko ya kweli siku zote huletwa na mapinduzi ya umoja wa kweli usio na kificho,woga,wala kulegalega!
katika ukurasa huu basi,tutapata nafasi  ya kushirikian kupeana habari kwa uwazi wa hali isiyo ya kawaida,usiobagua ila unaozingatia UKWELI TU!
karibuni "and lets make MTANZANIA MWENZANGU Tanzanias most read blogg!

No comments:

Post a Comment